Muda mfupi uliopita,Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Shirima ambaye
ni Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo jijini Dar es
Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo
ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi
zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.
Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangkia katika Gari
aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli
hiyo,chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika
mpaka sasa. Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi
uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa na mshtuko baada ya kusikika kishindo
cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia
ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja
la Shirima.
|