MAELFU WAHUDURIA MAZIKO YA MAREHEMU BI KIDUDE WAKIWEMO VIONGOZI WA WAKUU WA NCHI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein,
katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi
Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini
Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba
Wilaya ya Kati, Unguja.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu
Fatma Baraka 'Bi Kidude', wakati wakiingiza jeneza hilo Msikiti wa
Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea kijijini kwa
marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana huu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul Jumaa (kulia)'Diamond
Plutnum', akiwa ni mmoja kati ya wasanii waliohudhuria katika dua maalum
ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu
katika Msikiti wa Mwembeshauri, mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia
kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.
Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi R.I.P..........KIDUDE BINTI BARAKA
Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu bi Kidude, Zanzibar
Msanii Fid Q, Baraka cousin ya Marehemu Bi Kidude na Hassan Bond
Mussa (FID Q ndo alikuwa msanii wa kwanza mkubwa kufika msibani kwa
bibi)
Ruge mutahaba, Babu Tale and Guru. .......msibani kwa Bi Kidude
Guru G na Mh Bhaa mazikoni
Hassan na Fid Q wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Bi Kidude
Sehemu ya umati wa Watu waliofika msibani