IFUNDA:PAROKO APOTEZA MAISHA KWA AJALI MBAYA YA GARI

 


 

Hili ndilo gari ambalo limesababisha kifo cha paroko


PAROKO wa kanisa la RC parokia ya Ifunda Alphonce Mhamilawa amefariki dunia katika ajali mbaya ya gari iliyotokea katika eneo la Sabasaba Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Mashuhuda wa ajali hiyo wameueleza mtandao huu kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2 usiku wa kuamkia leo wakati paroko huyu akitoka mkoani Njombe katika shughuli ya Mazishi

Mmoja kati ya mashuhuda hao Bw Saugo Ndemo alisema kuwa paroko huyo alikuwa akiendesha gari dogo aina ya Toyota Hilux (Pick Up) yenye namba za usajili T434 APP mali ya Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Ifunda.

Ndemo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Paroko kuligonga gari aina ya Lori kwa nyuma na kuwa lori hilo halikuweza kusimama.

Alisema kuwa paroko huyo alifia eneo la tukio baada ya ajali hiyo iliyopelekea kichwa chake kupasuka.

Mmoja kati ya askari wa usalama barabarani ambae hakutaka kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji mkuu wa jeshi la polisi alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.

Pia alisema kuwa lori ambalo paroko huyo aliligonga linasadikika kuwa lilibeba mbao huku likivutana na lori jingine na baada ya ajali hiyo halikuweza kusimama.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family