Ngoma mpya kutoka kwa Diamond iliyovuja kupitia kwenye mitandao mbali
mbali "ukimuona" ambayo pia inasikika kupitia Club mbali mbali,
inasemekana kuwa ni demo, haikua imekamilika, lakini baada ya kupoteza
sim yake aina ya Blackberry iliyokua kwenye moja ya gari zake, ndio
imesababisha kuvuja kwa wimbo huo..
"kweli kabisa siku release na hiyo nyimbo hapo ilipo haijaisha kabisa,
hap katikati nilikua na sim yangu blackberry bold 4 niliipoteza bahati
mbaya ikaibiwa, nilikua natoka nyumbani naenda magomeni, nafika kariakoo
nakuta siioni sim. hasa katika sim mara nyingi nakuwa sometimes naweka
nyimbo, kwasababu moja ya gari yangu haina cd, nilikua sijaweka sound,
nikawa nasikiliza kupitia sim yangu nachomeka katika gari.ila kila kitu
kinachotokea kwangu sometimes namshukuru mungu kwasababu yeye ndio
anaandika, watu wanaipeda sana napoenda kwenye show zangu watu wanataka
niimbe..namshukuru sana mungu".
SOURCE:djfetty Blog