Marehemu Padri Evarist Mushi |
Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili
Zanzibar, Evarist Mushi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi saa 1.00
asubuhi na kufariki kabla hajafika hospitali ya Mnazi Mmoja.
Paroko huyu amepigwa risasi akishuka katika gari
lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00 leo.
Padri Evarist Mushi amepigwa risasi kichwani na
kufa papohapo na watu wasiojulikana akiwa njiani anaenda kuendesha misa katika
Kanisa la Mt.Theresia eneo la Mtoni Zanzibar.
Msemaji wa Jeshi Polisi Zanzibar Inspekta
Mohamed Mhina amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa padre huyo
ameuawa wakati akijiandaa kuingia kanisani akitokea kwenye gari yake ambapo
ndipo alipofikwa na umauti huo.
Jeshi la Polisi visiwani humo kupitia kwa Msemaji wake Mkaguzi wa Polisi, Mohamed Mhina limelaani mauaji hayo na na kusisitiza kuwa Jeshi limeanza msako mkali wa kuwabaini wauaji hao.
Hili ni tukio la pili kutokea Zanzibar ambapo
tukio la kwanza lilitokea kwa Padre Ambrose Mkenda kupigwa risasi na kujeruhiwa
na watu wasiojulikana.
Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Mahala Pema Peponi ..Amen