Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba
akizungumza na wasanii maeneo ya Amana wakati Matumaini akiwa kwa
daktari.
MSANII wa vichekesho ambaye alikuwa nchini Msumbiji, Tumaini
Mwakibibi ‘Matumaini’ jana alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya
kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar
akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo
kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na
kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya
Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu.
HABARI NA PICHA-GLOBAL PUBLISHERS
|