Baadhi
ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wanaoishi kwenye
Hostel za Mabibo,wakiangalia moja ya majengo ya Hostel hizo likiwa
limeshika moto asubuhi hii.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na
msaada wa haraka unahitajika ili kuokoa mali zilizopo kwenye Jengo hilo.
Hakuna anaeamini anachokiona,kwani imekuwa ni tukio la ghafla sana.
Baadhi
ya Wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye Jengo hilo wakiwa nje,huku
wakiwa hawajui la kufanya wakati moto huo ukiendelea kuwaka.
Moshi unazidi kufuka na moto unaongezeka.