Polisi wa Pakistan wanamsaka Ali Nawaz Leghari, ambaye ni baba anayekabiliwa na mashtaka ya kuua watoto wake watano kwa imani za kishirikina.
Mama wa watoto hao amesema alikuwa
akigombana na mume wake kutokana na kitendo chake cha kujihusisha na
masuala ya ushirikina, jaribio la kwanza la kuwawekea sumu watoto
wake kwenye chakula cha jioni lilishindwa baada ya mkewe kumshtukia.
Mwanamke huyo alifanikiwa kukimbia na
mtoto wake mmoja ambaye ni mkubwa na kuwaacha wengine watano ambao umri
wao ni kati ya miaka 15 na wa mwisho miaka 3 ambao aliwapa dawa ya
usingizi na kisha kuwanyonga.
Polisi walipofika kwenye nyumba hiyo walikuta miili ya watoto hao Haseena (15), Mukhtiar (12), Shabir (7), Humera (4) na Zameer (3),
baada ya kufanya mauaji hayo akichukua basi na kutoroka, huku mtoto
aliyenusurika akimwaambia Polisi kuwa baba yake ni muathirika wa dawa za
kulevya na alitaka kujihusisha na masuala ya kichawi.
|