Na Rose Masaka-MAELEZO
UKAWA
waombwa kukubali maoni ya watanzania walio wengi ya kuheshimu pesa za walipa
kodi kwa kurudi bungeni na kupingana kwa hoja kwani hoja zao zikiwa za huakika
hazitapingwa bali kanuni na taratibu zinazoendesha bunge zitafuatwa badala ya
kuendelea kulalamika katika majukwaa ya kisiasa.
Kauli
hiyo imetolewa na balozi wa amani Tanzania Risasi Mwaulanga alipokuwa akiongea
na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo leo jijijni Dar es
Salaam.
“Nawaomba
UKAWA warudi bungeni ili tuweze kupata katiba mpya itayoyokidhi changamoto za
watanzania wote na sio masuala ya vyama vya kisiasa na maslahi binafsi kwani
vyama hiyvo vinaweza kutoweka wakati wowote na nchi ikabaki palepale”.Alisema
Mwaulanga.
Aidha
Mwaulanga anaiomba iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya jaji Warioba,
viongozi wa dini, na asasi za kiraia kuendelea na jitihada za kuitaka UKAWA
kurejea Bungeni ili kurahisisisha upatikanaji wa Katiba mpya yenye maslahi
mapana kwa ummma kuliko ya kisiasa.
Balozi
huyo wa amani amesema kuwa kauli za vitisho na uvunjifu wa amani unapaswa
kupigiwa kelele na kulaniwa na kila mwanademokrasia duniani katika kipindi hiki
cha kuandaa Katiba mpya ili wajumbe waweze kuwa huru wakati wa kutoa maoni.
Tanzania
ni nchi ya amani,umoja, upendo na maelewano na siyo nchi ya vita,chuki na
mafarakano hivyo watanzania tunapaswa kutambua ni Katiba gani tunayoitaka na
kuwa na mtazamo sahihi na maamuzi bora.