Muimbaji mkongwe wa nyimbo za taratibu Celine Dion kutoka Canada,amelazimika kusitisha shughuli zote za muziki ili kumuuguza mume wake Rene Angelil anayesumbuliwa na kansa ya koo. Dion mwenye miaka 46 amefuta tour yake ya bara la Asia pamoja na kusimamisha show zingine zote ili apate muda wa kutosha kumuuguza mume wake. “I want to devote every ounce of my strength and energy to my husband’s healing, and to do so, it’s important for me to dedicate this time to him and to our children,” alisema Dion Jumatano wiki hii. Dion pia amewaomba radhi mashabiki wake:“I also want to apologise to all my fans everywhere, for inconveniencing them, and I thank them so much for their love and support”. Mwezi Desemba, 2013 Angelil mwenye miaka 72 alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye koo lake, uliopelekea kumpa wakati mgumu kwa sasa. Mwezi June Angelil alistaafu kuwa meneja wa Celine Dion baada ya miaka 30. Dion na mume wake waliingia kwenye uhusiano wakati Dion akiwa na umri wa miaka 19 na Angelil alikuwa na miaka 45, kwa sasa wana watoto watatu. |