MSIBA: MKE WA AFANDE SELE AFARIKI DUNIA

Picha ya familia: Kutoka kulia ni Asha Mohammed Shiengo ‘Mama Tunda’ enzi za uhai wake, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, Asantesana Selemani na Tunda Selemani.
MKE wa mwanamuziki Selemani Msindi ‘Afande Sele’, Asha Mohammed Shiengo 'Mama Tunda' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa Morogoro kwa ugonjwa wa Malaria. 
Marehemu aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro kabla ya mauti kumfika na mwili wake unatarajiwa kuzikwa leo saa 10 jioni katika Makaburi ya Kola mkoani humo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Afande Sele aliandika hivi baada ya msiba huo:
Akiwa na Afande Sele, Mama Tunda alijaliwa watoto wawili, Tunda Selemani na Asantesana Selemani. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. AMEN
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family