Muimbaji na mtunzi wa nyimbo, Barnaba Elias amedai kuwa baada ya
kumtumia mke wake ‘Mama Steve’ kama model kwenye video ya wimbo wake
‘Wahalade’, ameanza kupata usumbufu mkubwa kutoka kwa wasanii wengine
wakimtaka mke wake atokee kwenye video zao, kitu ambacho hawezi kuruhusu.
“Mimi niliamua nimtumie kwa mara moja tu kwa sababu mimi ni wife wangu,
sihuruhu mtu yoyote amtumie wala sipendi hata akawa na nini, mimi
sitaki,” ameiambia Bongo5. “Mimi nilimtumia kwa sababu niliona anafaa,
she is beautiful, nikaona acha ni mtumie kwa mara moja. Siruhusu mtu
kufanya hivyo na yeye mwenyewe anajua mimi sipendi mtu afanye hivyo.
Watu wapo wanaosumbua na mimi nawaelekeza sitaki mke wangu afanye hivyo
na ana biashara zake,” ameongeza Barnaba.
Wakimbizi wa TikTok waikimbilia App ya RedNote
2 hours ago