UJUMBE WA BILL GATE WAWASILI TFDA


 Ujumbe kutoka Bill & Melinda Gates Foundation umefanya ziara Tanzania na kuitembelea pia TFDA kwa lengo la kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya afya wanayoifadhili Tanzania. 

Ujumbe huo unaoongozwa na Mkurugenzi katika Mfuko huo Bw. Michael Poole, umesifu maendeleo ya Mradi wa ADDO na Uwianisho wa mifumo ya udhibiti wa dawa kwa nchi za Afrika Mashariki, miradi ambayo TFDA imekuwa ikisimamia utekelezaji wa ADDO hadi mwaka 2012 na kushiriki Uwianisho wa mifumo ya udhibiti wa dawa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki toka mwaka 2012 hadi sasa. 

Hivi sasa ADDO inasimamiwa na Baraza la Famasi kufuatia Sheria ya Famasi ya mwaka 2011.Wenyeji wa ujumbe huu ni Shirika la Menejimenti ya Sayansi ya Afya (MSH) ambao ni wadau wakuu wa mradi wa mpango wa ADDO nchini.
  Picha ya kikao cha ueasilishaji wa taarifa za maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Mfuko huo

 Picha ya pamoja ya ujumbe kutoka Mfuko wa Bill & Mellinda Gates, Maafisa wa TFDA, MSH na Baraza la Famasi mara baada ya ziara ya TFDA.
Picha ya Kaimu Murugenzi Mkuu TFDA, Dkt. S.S Ngendabanka, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Mfuko wa Bill & Mellinda Gates Bw. Michael Poole katika viwanja vya TFDA
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family