Kiasi
cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli
wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na
moto leo (Jumatano) asubuhi.
Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani.
Hakuna
mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea.
Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kilifika wakati tayari mabweni hayo
yameshateketea.
Mbunge
wa Jimbo la Monduli Mh Edward Lowassa ametembelea shule hiyo na
kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati utaratibu
unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.
Gharama
za kuwasafirisha wanafunzi hao ni shilingi laki Saba. Aidha Mh Lowassa
amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa
magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
Kikosi Cha zimamoto kikijaribu kupambana na moto ulioteketeza mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli.
Mbunge
wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya
Erikisongo mjini Monduli yaliyoteketea kwa moto, akiongozana na mkuu wa
shule hiyo mwalimu Agnes Nyange.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo Monduli mjini yaliyoteketezwa kwa moto.
Mbunge
wa Monduli Mh Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa afisa elimu wa
Monduli mwalimu Shaaban Mgunya wakati alipotembelea mabweni ya shule ya
sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli yaliyoteketea kwa moto.