![]() |
| Dkt Cheni Akiwa Kitandani Hospitalini Alipolazwa |
Msanii wa filamu nchini, Dr Cheni amelezwa toka jana katika hospitali ya Buruhani jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa Dengue.Akizungumza na Bongo5 leo Dr Cheni amesema kuwa bado hali yake sio nzuri kutokana na kuishiwa damu na mwili kupoteza nguvu.
![]() |
| Dkt Cheni Akiwa Na Mmoja Wa Waigizaji Wenzake Wengi TUnamjua Kwa Jina La Jb Aliyefika Hospitalini Hapo Kumjulia Hali |
“Bado ni nipo hospitali ya Buruhani naumwa hili gonjwa jipya,sijui unaitwa Dengue,” amesema. “Bado hali yangu sio nzuri kabisa,yaani naumwa,napungukiwa damu,mwili unauma,kwahiyo yani bado ninaumwa,hii homa ilinianzia wiki iliyopita sema nilikuwa bado hawajaigundua ila jana ndio wameingundua,” ameongeza.
Dr Cheni amesema kuwa anawaomba Watanzania wamuombee kwani bado hali yake sio mzuri.
![]() |
| Dr Cheni akipewa huduma na msanii mwenzake wa filamu |



