BAADA YA SHEDDY CLEVER KUKOSA TUZOMHIKI NDICHO ALICHOKISEMA MASTER J


Baada ya tuzo za KTMA kumalizika kila mmoja amekuwa na mtazamo wake,Wiki hii Producer wa wimbo wa ‘Number One’ wa Diamond, Sheddy Clever alitoa malalamiko yake ya kukosa tuzo ya mtayarishaji bora huku wimbo alioutengeneza ukimpa Diamond zaidi ya tuzo tano.

Producer mkongwe Joachim Kimaryo aka Master J ametoa mtazamo wake kuhusu Tuzo za KTMA 2014 ambao unaonesha hakuridhishwa na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa mwaka – kizazi kipya ambaye ni Man Water wa Combinenga. 


“Sijaelewa damond kupata tuzo 7 alafu produza wake kutoka na 0!!!!!” ni jibu la moja ya maswali kuhusiana na tuzo hizo aliyokutana nayo Master J Jana alipokuwa mgeni katika session ya ‘Kikaangoni Live’ kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV.




 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family