DIAMOND NA MSANII PROFESSOR KUTOKA SOUTH AFRIKA KUSHAMBULIA JUKWAA KATIKA ZIARA -ROAD TO MAMA

Diamond (2)
Damond Platnumz Msanii Kutoka Tanzania

Msanii Professor Kutoka South Afrika

Zikiwa zimesaliya siku chache za utoaji wa tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMA) 2014, msanii Diamond ambaye pia ni mshiriki wa tuzo hizo pamoja na msanii Professor kutoka Afrika Kusini wanatarajia kupanda jukwaani kutumbuiza katika sherehe ya uhamasishaji wa utoaji wa tuzo hizo siku ya tarehe 16 May ndani ya ukumbi wa club Bilicanas.

Mbali na wasanii hao pia kutakua na ma DJ wakali kutoka nchi mbalimbali ambao watatoa burudani katika sherehe hiyo ya uhamasishaji wa tuzo za MAMA, ma DJ hao ni pamoja na DJ Zero, DJ Steve B, DJ Mafuvu wote kutoka Tanzania na DJ Tira kutoka Afrika Kusini ambae pia ni DJ wa kituo cha Televisheni cha MTV Base.

Sherehe hizo zinalenga kuhamasisha wananchi katika kushiriki kikamilifu katika tuzo hizo na kwa nchini, zitafanyika Club Bilicanas , katika jiji la Dar es Salaam na Ticket zitauzwa mlangoni kwa bei ya shilingi 15,000 kwa mtu moja, mwezi ujao wasanii wataelekea jiji Lagos Nigeria kwa ajili
ya uhamasishaji.


Vilevile wasanii kutoka Afrika Kusini akina mafikizolo na Davido wa Nigeria wamependekezwa kwenye vipengele vingi zaidi ya moja, wamependekezwa katika vipengele vinne muhimu, hivyo wameumana katika kuwania tuzo za msani bora wa mwaka pamoja na wimbo bora wa
kushirikishwa pia.

Pia kutakua na washiriki wawili ambao ni Radio na weasel wa Uganda , na
Kenya msanii Amini kupitia wimbo wake wa kiboko changu alioshirikiana na
Radio and Weasel nao utashindanishwa.

MTV leadership award, ni tuzo inayo lenga vijana wa Afrika wanaume na
wanawake wenye umri mdogo mpaka miaka 40 ambao wanafanya vizuri kwenye
mambo mbalimbali ikiwemo muziki biashara na science. MTV pia inatambua
mafanikio ya muzkik na wana muziki ambao wana wakilisha Afrika nchini na
nje ya Afrika.

MAMA 2014 itausisha wasanii wa Afrika na wa Kimataifa pamoja ikiwa
pamoja na tuzo ‘sahihi kwa kushirikiana kati ya wasanii wa muziki na
tamaduni mbalimbali.

Upigaji kura MTV Africa Awards uko wazi kwenya www.mtvbase.com kuanzia 16 April 2014 mpaka usiku wa manene 4 Juni 2014. Kwa maelezo Zaidi juu ya MTV Afrika Muziki Awards kwaZulu –Natal, tembelea tovuti www.mtvbase.com, like us on Facebook at www.Facebook.com/MTVBaseVerified, or follow us on Twitter @MTVBaseAfrica. To join the conversation about the awards please use the hashtag #MTVMAMA.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family