MAGONJWA YA MLIPUKO YANUKIA DAR

IMG-20140107-WA0007
Picha juu na chini ni magari ya kuzolea taka ngumu ya kampuni mbalimbali yakiwa kwenye foleni ya kuingia Dampo la Pugu Kinyamwezi ambalo miundo mbinu yake ni mibovu na kupelekea zoezi hilo kuchukua zaidi ya siku 4 mpaka kufanikisha kufikia eneo maalum la kumwagia taka ngumu.

.Ni kutokana na kukwama kwa magari ya taka kwenye Dampo la Pugu
.Siku ya tatu sasa magari ya taka yamekwama

Na.Mwandishi wetu, MOblog
MIUNDOMBINU mibovu katika Dampo kuu la jiji la Dar es Salaam Pugu Kinyamwezi imesababisha magari makubwa ya kuzoa na kumwaga taka kukwama kwa muda wa siku tatu na kupunguza ufanisi wa kuzoa taka katika mkoa wa Dar es Salaam, MOblog inaripoti.
Mtoa taarifa wetu ambaye hakutaka kutajwa kwenye blogu hii, amesema kwamba uongozi wa Dampo Pugu umeshidwa kuweka utaratibu mzuri na kukarabati miundombinu ya dampo kwa muda mrefu na kusababisha msongamano mkubwa wakati wa kwenda kumwaga taka katika sehemu hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa MOblog jana asubuhi, mtoa taarifa (Jina linahifadhiwa) amesema kwa muda wa wiki mbili sasa umwagaji wa taka katika dampo hilo siyo mzuri kabisa na inaweza kufika miezi kadhaa tangu dampo hilo lianze kuelemewa na uchafu kutoka kila kona ya jiji la Dar es Salaam.

“hali ni mbaya katika dampo la pugu kwa miezi kadhaa sasa na uongozi wa dampo wameshidwa kufanya kazi kwa tija na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa dampo katika jiji la Dar es Salaam,’ amesema mtoa taarifa.

Amesema magari makubwa aina ya (Bulldozers) hayawafanyi kazi kabisa na kusababisha kukwama kwa kazi ya kumwaga taka katika dampo la Pugu Kinyamwezi na msongamano mkubwa wa magari. Mtoa taarifa anasema kuwa kutokana na matatizo hayo katika dampo la Pugu imesababisha baadhi ya taka kuoza kabisa na kuleta harufu kali kwa wakazi wa karibu wa dampo hilo na tishio la magonjwa ya mlipuko ni kubwa. “kutokana na tatizo hili katika dampo la hapa Pugu hali za kiafya kwa wakazi wa karibu wa eneo ni ya hatari na magonjwa ya mlipuko yako mbioni kutokea,” aliongeza.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family