![]() |
| Marehemu |
Ni kifo cha kusikitisha cha mwanamke
huyo pichani Hamida Urembo na muhusika wa mauaji hayo ni mumewe wa ndoa
waliyeishi kwa miaka mitatu. Hamida alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu na
mwaka watatu na alikuwa anatarajia kugraduate mwezi huu chuoni hapo.
Hamida na mumewe Yahaya walibahatika kupata mtoto wa kike mwenye miaka mitatu sasa.Kwa mujibu wa dada wa Hamida ndoa yao ilikuwa ya misuko suko sana.Mume alikuwa sio mwaminifu mara nyingi alikuwa akizini nje.Ukiacha hilo alikuwa akimpiga sana mkewe mpaka kumzimisha.
Hamida na mumewe Yahaya walibahatika kupata mtoto wa kike mwenye miaka mitatu sasa.Kwa mujibu wa dada wa Hamida ndoa yao ilikuwa ya misuko suko sana.Mume alikuwa sio mwaminifu mara nyingi alikuwa akizini nje.Ukiacha hilo alikuwa akimpiga sana mkewe mpaka kumzimisha.
![]() |
| Huyu ndiye Yahaya aliyekuwa mume wa marehemu Hamida |
Matatizo ambayo ndugu walikuwa wakiyajua na walishasuluhisha mara nyingi na Hamida kurudi kwa mume kuendelea na maisha.Hii ya mwisho ndio ilikuwa kubwa zaidi.Mume alikuwa akimtongoza housegirl hapo nyumbani na alipokuwa kesho housegirl akamfahamisha mama.
Akamueleza jinsi gani muwewe amekuwa
akimsumbua kumtaka kimapenzi.Hamida akamwambia anataka tu uthibitisho
kama ni kweli.Siku ya siku Yahaya akamlazimisha Hamida kwenda kwao na
Hamida akakubali akijua kuna jambo.Akasindikizana na mumewe mpaka
kituoni mume akijua mkewe hayupo kumbe mke aligeuzia njiani akarudi
nyumbani akajificha chini ya uvungu chumbani kwa housegirl wake.Baadae
mume akawasilia na housegirl kuwa anarudi nyumbani,aliporudi akaendelea
kuomba mambo tena akavua nguo kabisa akabaki na boxer.Wakati huo yupo
chumbani kwao na mkewe.Housegirl akamwambia wahamie chumbani kwako hapo
sio salama.Basi wakahamia chumbani na akawa ndio anamuinamisha dada ili
amfanye Hamida akatoka chini ya uvungu ili kumuokoa dada na kumuonyesha
mumewe kuwa alikuwepo na amejua usaliti wake.Na alipokuwa chini ya
uvungu alikuwa akirekodi kila kitu kwenye simu na alipotoka na picha
akapiga.
Hamida alitoka hapo akashitaki kwao na
kwao wakamwambia aende kwa mjomba wa mumewe kumueleza matatizo ya mtoto
wao. Alipofika kwa mjomba akaambiwa wanaume ndivyo walivyo avumilie tu
arudi kwa mumewe.
Hamida akarudii kwao akiwa hana hana
raha lakini uamuzi aliouchukua ni kuachana na mumewe kwani alikuwa
kashachoka. Wakawa wakivutana sana mume akimsihi arudi nyumbani
walikokuwa wakiishi Mbagala ila Hamida hakuridhia.
Hamida alishaenda mpaka Bakwata ili mumewe aamriwe kutoa talaka.
Mwisho wa Hamida kuonekana nyumbani ni
siku ambayo yeye na ndugu zake walikuwa waende kijijini kwao kwenye
viwanja walivyopewa na babu yao.Ila siku hiyo Hamida alitoa udhuru kuwa
haendi na akamtaarifu mama yake kuwa Yahaya kamuita akachukue vitu vyake
vilivyobakia.Mama akamkatalia kwenda akamwambia kuna kaka zake wakubwa
aache wataenda kuvifata kwani huyo mume ni mshenzi anaweza kumfanyia
kitu kibaya.Hamida akamwambia mama anataka kwenda mwenyewe kwani kuna
vyeti vyake muhimu akavichukue.
Basi mama akamuacha aende kishingo
upande lakini mama akamwambia basi nenda hata na mdogo wako.Akaenda na
mdogo wake lakini kufika kule mume akamkatalia mdogo mtu kuingia ndani.
Wakabishana sana kwa nini asiingie mdogo
mtu kuepusha shari akaenda kukaa kwa jirani asubiri kuitwa. Akakaa na
muda kupita kukawa kimya akajua wale wameelewana ndio maana hakuna
makelele hivyo akaendelea kusubiri.
Akakaa weee mpaka jioni giza lilipoanza
kuingia kidogo Yahaya akampigia simu kwa kutumia simu ya Hamida
akimwambia aondoke tu arudi nyumbani wao wameshaondoka na vyombo
wamebeba.
Mdogo mtu akaondoka kurudi nyumbani kwao Tabata akijua mke na mume wameelewana kumbe dada yake ameshakufa ndani.
Mdogo mtu akafika nyumbani saa mbili
usiku na kumwambia mama jinsi Hamida alivyomuudhi kamuacha yeye kwa
jirani na akaondoka na mumewe Yahaya.Mama machale yakamcheza akanyanyua
simu akampigia Yahaya kumuuliza mwane yupo wapi.Yahaya akamjibu kuwa
ameachana nae kitambo mama akamwambia sio kweli mwanangu hawezi
kuchelewa kurudi nyumbani na hana kawaida hiyo.Yahaya akamjibu atarudi
tu Hamida mtu mzima.
Mamam tayari alishajua kuna jambo
akampigia simu baba Hamida aliyekuwa Arusha kumtaarifu kilichotokea.
Baba Hamida akampigia Yahaya lakini hakupokea simu.Wasiwasi ukazidi
kutanda na ndugu kupeana taarifa zaidi.Asubuhi kulipokucha wakaenda
Mbagala kwa Yahaya lakini wakatoa taarifa polisi.Polisi wakawaondoa
wasiwasi kwamba hao wanajuana wenyewe labda wameamua kukumbushiana.
Ndugu hawakuridhika wakaenda kwa mjumbe
awaruhusu wavunje nyumba waingie ndani pengine kamfungia ndani maana
ilikuwa kawaida yake kufanya hivyo kumfungia Hamida ndani.Basi mjumbe
akaruhusu mlango uvunjwe walipoingia ndani palikuwa patupu hawakuona
kitu wala dalili za mauaji.Kuna chumba ambacho ni stoo hicho walishindwa
kufungua na mjumbe akawaambia hiyo ni stoo wanawekaga mavitu yamejazana
humo basi wakakiacha wakaondoka.
Hawakuishia hapo bado waliendelea kumsaka Hamida bila mafanikio.
Hamida alipotea toka jumapili
iliyopita,jumanne juzi kila mtu wakapanga kila mtu akamtafute popote
pale anapoona anaweza kumpata.Mama akaenda kwenye maombi kanisani wakati
muislam,dada akaenda blue pearl kazini kwa Yahaya na huku majirani
Mbagala wakaanza kuona inzi na harufu kali ikitoka nyumbani kwa
Yahaya.Ikabidi mjumbe apige simu kwa mama Hamida kumueleza
kinachoendelea polisi wakaitwa,nyumba ikavunjwa ili kutafuta harufu
inatokea wapi.Wakavunja kile chumba cha stoo na kukuta mwili wa Hamida
umeshaanza kuharibika.Kanyongwa na kamba ya katani na kitenge kafungwa
puani na mdomoni.Mwili wake ukawekwa kwenye mfuko akajaziwa mito na
manguo nguo na tendegu la kitanda kawekewa shingoni.
Ndugu, polisi wakachukuwa mwili kwa ajili ya msiba na mazishi wakati huo Yahaya alishakimbia siku nyingi hajulikani alipo.
Hamida alizikwa jana kule kwa babu yake
Mzenga uzaramuni walipokuwa waende kwenye mashamba waliyopewa. Msiba
upo nyumbani kwao Tabata. Mrehemu ameacha mtoto wa kike wa miaka mitatu
anaitwa Tayana.
Habari hii inaendelea tena kesho katika heka heka za leo ndani ya leo tena ya clouds fm.
Na kwa sasa kama nilivyo report hapo mapema leo kwamba mthumia Yahaya anatafutwa na police kwa kosa la mauwaji ya mkewe Hamida.
R.I.P Hamida na tunatoa pole kwa familia nzima ya Urembo kwa msiba huu.
Source: Dina Marios


