YULE MBUNGE SHAROBARO WA KENYA ASHINDA KITI CHA UBUNGE KWA MARA NYENGINE

..
Sonko
.
Pamoja na Usharobaro wake, Gideon Mbuvi maarufu kama Sonko… yule mbunge aliependwa na wengi na anaejichanganya sana na watu wa kipato cha chini ametangazwa mshindi wa kiti cha Useneta wa Jiji la Nairobi Kenya ambapo alitoa machozi kwa kutoamini kama kweli ameshinda.
Hiyo picha hapo chini japo haionekani vizuri inamuonyesha Sonko wakati akitangazwa mshindi, alikua kapiga T shirt yake ya njano, kofia na hereni pia kama kawaida… alafu kwenye mkono akatupia pete kadhaa za gold pamoja na saa kubwa mkono wa kushoto.
Sonko ambae amepata umaarufu kwa Usharobaro wake pia ambao ulimfanya kuwa Mbunge wa kwanza kwenye historia ya Kenya kuingia bungeni amevaa hereni, ameshinda kwa kupata kura zaidi ya laki nane wakati mpinzani wake Wanjiru aliepata kura laki tano.
Sonko ni mtu wa kujichanganya sana, nakumbuka hata wakati ule Z Anto wa Binti kiziwi yuko juu kwenye chati, Sonko alimpatia usafiri pamoja na walinzi wa kutembea nae wakati alipoalikwa kwenye kupafom Kenya.
.
          Akijielezea baada ya Matokeo         



 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family