HABARI KUHUSU MHARIRI ALIYETOBOLEWA JICHO NA KUUMIZWA VIBAYA NA WATU WASIOJULIKANA


Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
nchini na Mhariri Mtendaji wa New
Habari Corporation Absalom Kibanda
usiku wa kuamkia march 6 2013
ameshambuliwa na watu
wasiojulikana na kuumizwa vibaya na
baadhi ya viungo vyake kunyofolewa.
Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri
Theophil Makunga amesema tukio
lilitokea saa sita usiku wakati kibanda
alipokua akiingia nyumbani kwake
akitokea kazini, alipiga honi geitini ili
afunguliwe na mlinzi ndipo lilipotokea
kundi hilo na kuvunja vioo vya gari na
kuanza kumshambulia.
Baada ya mlinzi kupiga kelele kuomba
msaada ndipo kundi hilo lilipokimbia
huku tayari likiwa limemng’oa jino
Kibanda pamoja na kumtoboa jicho la
kushoto ambapo kwa sasa inasubiriwa
ripoti ya Madaktari wa Taasisi ya
mifupa (Moi) ambako amelazwa.
Afisa Mtendaji wa New Habari Hussein
Bashe amesema baada ya kukamilika
kwa mpango wa kufatilia hati ya
kusafiria ya Kibanda ambayo Serikali
iliizuia kama dhamana ya kesi
inayomkabili, wanatarajia kumpeleka
Afrika Kusini kwenye hospitali ya Mil
Park.
Kamanda Suleiman Kova wa Kanda
maalum ya Dar es salaam amesema
Polisi imeteua maafisa wanne wenye
uzoefu wa ishu za upelelezi ambao
watashirikiana na maafisa kutoka
makao makuu ya jeshi hilo kufanya
uchunguzi.
Pamoja na hayo, Waziri wa mambo ya
ndani Dr. Emmanuel Nchimbi nae
amezungumzia hili tukio kwa kusema
Serikali inalaani vikali hilo tukio na
itatumia nguvu zake zote kuwasaka
waliohusika.

 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family