![]() |
Boniface Wambura
|
Na Mwandishi Wetu
WADAU watatu wa mpira wa miguu wamechukua fomu za
kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kufanya
idadi ya waliojitosa katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24
mwaka huu kufikia 30.
Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika
ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya
www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili
alasiri Januari 18 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Waliochukua fomu
leo Januari 16 mwaka huu kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa
TFF, Athuman Jumanne Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo.
Mwengine aliyechukua leo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TFF kuwakilisha Kanda ya Iringa na Mbeya.
Orodha kamili ya wadau waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni
Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo
(urais), Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (umakamu wa
rais).
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye
mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel
Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo
na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora),
Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na
Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima
(Dodoma na Singida), Farid Nahdi na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani),
Elias Mwanjala (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga)
na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).
Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu kwenye
ofisi za TFF mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya
uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu
mwenyekiti.
Wakati huo huo; WAHARIRI na
Waandishi wa Habari zaidi ya 40 wameshiriki kwenye semina kuhusu Kanuni
za Uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyofanyika
leo Januari 16 mwaka huu.
Wawezeshaji katika semina hiyo iliyofanyika ofisi za TFF walikuwa
Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Deogratias
Lyato na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.
Short URL: http://www.thehabari.com/?p=27538

