KAZI YA KUTULIZA GHASIA ZA MAANDAMANO ILIVYOKUWA KWA WANAFUNZI WA IFM KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM.
| Alichagua kama maembe au mpira na kuchezea alivyotaka! |
BAADA ya
wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako
Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka
wakawasilishe hoja zao hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya
wahalifu na hayajashughulikiwa, waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja
vya mpira eneo la Machava nakutaka mkutano huo ufanyike kwenye kituo
cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi wengi wao walielekea huko.
Mara
baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende
kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu
yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na
kuumia wengine walipoteza fahamu.
Hata
hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano
huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo
la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa
watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu.
| Askari wa kike na wakiume wakimdhibiti kwa bakora na marungu mwanafunzi wa chuo cha IFM (mwenye nguo za blue) baada ya kumchomoa kwenye jengo alilojificha ili kukwepa mabomu ya machozi. |
| Mwanafunzi huyu alilala kabisa na kupoteza fahamu baada ya kuzidiwa na moshi wa mabomu ya machozi yaliyopigwa kwenye eneo la kituo hicho cha Polisi. |
| Mwanafunzi huyu alidondoka kwenye Difenda baada ya Defenda hilo kujazana wanafunzi wengi ambao wakipelekwa kwenye kituo cha Polisi Kigamboni. |
| Baada ya kitikisa mabomu yakutosha kwenye baa pembeni ambako walijificha wanafunzi hao walitaka amani itawale huku wakikimbilia gari la polisi ili wajisalimishe. |
| Huyu alishikiliwa mapema mara baada ya mabomu kuanza kupigwa, huku akionja joto ya jiwe ya askari hao ambao walionekana kuwa na uchu wakupiga. |
| Hapa amri ilikuwa ni mwendo wa kutembea kwa magoti lakini kipigo cha bakora kililazimisha wengine kuwaruka wenzao ama kuwakanyaga wale waliochini. |
