![]() |
| Rais Jakaya Kikwete . |
“Serikali haitavumilia vurugu wala
ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini
zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna
yeyote ile, inatosha,” alisema Rais Kikwete.
SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna
yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake
zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana.
Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia
wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa
gharama za kuligawa taifa.
Akizungumza
na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika
sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa
akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya
Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.
“Serikali haitavumilia vurugu wala
ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini
zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna
yeyote ile, inatosha,” alisema Rais Kikwete.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi
wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
(DRC), Juma Mpango alisema jumuiya ya mabalozi imefurahishwa na namna
ambavyo Serikali imekuwa ikishughulikia vurugu za kidini ambazo
zilitaka kujitokeza bila kusababisha madhara kwa wananchi.
“Tumeridhishwa na namna ambavyo
Serikali imekuwa inashughulikia mambo yake vizuri. Tunaomba mwendelee
kushughulikia amani ya nchi hii maana ndiyo mhimili wa nchi za Maziwa
Makuu,” alisema Balozi Mpango.
Kuhusu gesi
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.
Wakati Rais Kikwete akitoa kauli hiyo
jana, habari kutoka Mtwara zilidai kuwa Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, George Simbachawene amewekewa magogo barabarani kumzuia asiende
kwenye kijiji kinachozalisha gesi hiyo, huku Mkuu wa Wilaya ya
Nachingwea, Regina Chonjo akizomewa.
Hata hivyo, polisi walikiri wananchi
kuweka magogo barabarani kwa lengo la kumzuia waziri huyo, lakini
ikaeleza kuwa gari lililozuiwa siyo la Simbachawene.
Akizungumza na Balozi Corner, Rais
Kikwete alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia suala
la rasilimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujitafutia umaarufu wa
kisiasa na kuwapotosha wananchi.
“Ni jambo la hatari na lisilo na tija
kwa wanasiasa kujaribu kuigawa nchi vipandevipande kwa sababu ya
kujitafutia umaarufu kwa kutumia rasilimali za taifa,” alisema Rais
Kikwete na kuongeza:
“Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa
moja wakati kila mmoja anadai rasilimali kutoka kwenye eneo moja ibakie
na kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye
umoja wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa
kule Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba,” alisema Rais
Kikwete na kuongeza:
“Kwa
sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara
tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara, bali
ni watu wa Msimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60
kutoka Mtwara, kilomita 200 kutoka Newala.”

