
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akijaribu kumhadaa beki wa
Black Leopard, Ernort, wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa
kirafiki, unaoendeea muda huu katika Uwanja wa Taifa. Hadi sasa Yanga
inaongoza kwa mabao 3-1, bao la pili la Yanga limefungwa na Frank Dumayo
na bao la tatu limewekwa kimiani na Jerry Tegete katika kipindi cha
pili.

Kikosi cha Yanga. Timu ya Yanga inaongoza kwa bao 1-0 bao lililofungwa
na Jerry Tegete, kwa mkwaju wa penati, baada ya mchezi wa Yanga, Haruna
Niyonzima, kuangushwa katika eneo la hatari, wakati akiwatoka mabeki wa
Black Leopards.

Kikosi cha Black Leopards.

Mchezaji wa Yanga, Kabange Twite (kushoto) akimiliki mpira huku
akidhibitiwa na beki wa Black Leopards, Nkosiabo Xakane, wakati wa
mchezo huo.

Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao lililofungwa na Jerry Tegete.
