MOJA YA JENGO LA MABIBO HOSTEL JIJINI DAR LILIVYOSHIKA MOTO LEO ASUBUHI

Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wanaoishi kwenye Hostel za Mabibo,wakiangalia moja ya majengo ya Hostel hizo likiwa limeshika moto asubuhi hii.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na msaada wa haraka unahitajika ili kuokoa mali zilizopo kwenye Jengo hilo.
Hakuna anaeamini anachokiona,kwani imekuwa ni tukio la ghafla sana.
Baadhi ya Wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye Jengo hilo wakiwa nje,huku wakiwa hawajui la kufanya wakati moto huo ukiendelea kuwaka.
Moshi unazidi kufuka na moto unaongezeka.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family