WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. GEORGE SIMBACHAWENE ARIPOTI OFISINI LEO

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (kushoto) akizungumza  na waandishi wa habari mara baada ya kupokelewa na  uongozi wa  Wizara  hiyo. Kulia ni  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava. Mhe. Simbachawene amesisitiza umuhimu wa sekta za nishati na madini  kama mhimili  mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta za nishati na madini.
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (kushoto) akipokea ua   la maua kutoka kwa mmoja wa watumishi wa Wizara  ya Nishati na Madini  Lilian Aroko mara baada ya kuwasili  kwenye ofisi za   Makao Makuu ya Wizara  ya Nishati na Madini.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe.  Charles Mwijage (Kulia) akimpokea  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (kushoto) mara waziri huyo alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Wizara  ya Nishati na Madini.
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya  Sheria, Salome Makange  mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Makao Mkuu ya Wizara.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family