WACHEZAZAJI WA MPIRA WA KIKAPU WANAOINGIZA MKWANJA MREFU ZAIDI KWA MWAKA 2015

Lebron
Mchezo unaopendwa zaidi ya michezo mingine Marekani ni Basketball, ni kawaida kukutana na mastaa kama Jay Z na Beyonce wake, Kanye West na Kim Kadarshian wake, Lil Wayne, Floyd Mayweather, 50 Cent na wengineo wakijienjoy kuangalia mchezo huu.
Hapa nimekuwekea hii list ya mastaa ambao wameshasign kupokea pesa nyingi zaidi kwa mwaka 2015 Marekani!

le
No. 1: Lebron James, anaingiza dola za Marekani 64.6 (zaidi ya bil.119 Tshs), hizi zinatokana na mshahara anaolipwa na Timu yake ya Cleveland Cavaliers pamoja na deal za mikataba ya biashara ikiwemo ubalozi wa Beats by Dre.

kevin
No. 2: Kevin Durant, MVP wa 2013-14 ligi ya NBA, pato lake mwaka ni dola mil. 54 (zaidi ya bil.98 Tshs), hii ni makusanyo ya mshahara wake  anaolipwa Oklahoma City  Thunder na deal nyingine ikiwemo biashara ya matangazo ya Nike.

kob

No. 3: Kobe Bryant, anapokea dola mil 49.5 (zaidi ya bil. 89 Tshs), mshahara wake ni dola mil. 23 LA Lakers pamoja na kiasi kingine anachokusanya kwenye deals nyingine.
der
No. 4: Derrick Rose, anapokea kiasi cha dola mil. 38.9 (zaidi ya bil. 69 Ths) kutokana na mshahara dola mil.18 anaolipwa Chicago Bulls na dola mil. 20 za deal za Adidas, Powerade na nyinginezo.

car

No. 5: Carmelo Anthony, anaingiza dola 30.5 ( bil. 55 Tshs), mshahara wake ni dola mil. 22 anaolipwa New York Knicks nyingine ni kutokana na biashara nyingine
.
dw
No.6: Dwyane Wade, anaingiza dola mil 27 kutokana na mshahara wake Miami Heat pamoja na madili mengine.

amar

No.7: Amar’e Stoudemire, ni mchezaji wa New York Knicks pia, yeye anaigiza jumla ya dola 26.4 ( sawa na bil. 49 Tshs)
chr

No.8: Chris Paul, mmoja ya wachezaji wakali LA Clippers, kipato chake mwaka huu ni dola mil 26.1 (sawa na bil. 47 Tshs)
dwit

No. 9: Dwight Howard, kipato chake mwaka huu 2015 ni dola mil 25.9 (kama bil 47 Ths) ambazo ni mshahara wake Houston Rockets pamoja na mikataba ya biashara za matangazo.
blake

No.10: Blake Griffin, anaingiza dola mil 24.7 ambazo ni sawa na bil 48 mwaka huu, mshahara wake ni bil. 48 Tshs ndani ya LA Clippers.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family