Diamond
Plutnumz bado ameendelea kudhihirishia ulimwengu kwamba anapiga hatua
kulingana na juhudi alizonazo kwenye muziki,hili ni shavu lingine,kwa
sasa Diamond ameteuliwa kuwa moja kati ya wasanii wanaootoka Afrika na
watakaoshiriki katika Tuzo za muziki zitakazofanyika huko Eisemann
Center Dallas Nchini Marekani
Tuzo hizi zinatarajiwa kufanyika July 26 2014 na pia inategemewa
kuwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka Africa Magharibi Kusini na
sehemu zingine na taarifa iliyopo ni kwamba Mc wa shughuli hiyo atakuwa
ni mchekeshaji kutoka Nigeria Basket Mouth pamoja na Na Mrembo Pia
Muigizaji Kutoka Nollywood Juliet Ibrahim.
|
Show
hiyo inategemewa kuanza saa 2 kamili usiku na hii ni miongoni mwa show
kubwa kwa wa Africa maana Itakusanya wadau kibao wa muziki wa kiafrika
Duniani kutakua na Wanamuziki,Ma producer,Ma Manager,Dj’s Na kila
anaeendeleza Tamaduni za Kiafrica.
Unaambiwa pia Wageni kutoka Mataifa 17 ya Africa wanatarajia kutoka
Miji ya mbali mbali ya Nchini Marekani kuhudhuria Tuzo Hizo Ambapo kwa
hapa Tanzania tunatarajia kuwakilishwa na Diamond Platinum.
Diamond pia wiki chache zilizopopita alitoa Sample ya ClothingLine yake yenye nembo ya Wasafi Classic Baby.
|
Hizi ni sekunde kadhaa Diamond akielezea mchakato huo wa tuzo hizo.