| ‘Hizo picha hazina uhusiano
wowote unaounganishwa kimapenzi kati yangu na Ngassa ila ni sehemu ya
vipande vya movie yangu inaitwa ‘Majanga’ ambayo nimeanza kuifanya na
Ngassa amecheza ndani yake kwenye scene za mapenzi, yani Snura kwenye
movie amecheza kama binti mrembo anaerukiarukia Wanaume’ ‘Simu yangu
ilipotea ndio maana wamezipata hizo picha, wakati tunashoot tulikua
tunapigapiga tu hayo mapicha, mi sikuwa nataka kuzitoa kabisa manake
movie yenyewe bado naifanya nusunusu kutokana na kukosa muda, hii ishu
imeniletea sana matatizo manake mwingine anakua haamini unachokiongea na
hakuna kitu kinauma kama kuongea ukweli alafu mtu anasema unadanganya’ –
Snura Kwa kumalizia Snura anasema ‘Ngassa alinipiga muda mfupi tu baada
ya picha kuanza kusambaa akauliza mbona hizi picha zinasambaa hivi
Snura? nikamwambia usinielewe tofauti babaangu kwa sababu mimi mwenyewe
sikutaka zitoke, picha nilizopiga nyinginyingi tu wakati tunatengeneza
movie ila naona watu wameona hizi ndio nzuri kwa skendo’ |