| Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves-Le Drian
alisema jana kuwa wanajeshi hao watahudumu nchini humo kwa miezi sita
hivi. Kwa sasa Ufaransa ina wanajeshi 400 katika mji mkuu Bangui. Kikosi hicho cha walinda amani kilichoko nchini humo ni 2,500, na inategemewa kitaongezwa kufikia 3,500. Umoja wa Afrika utachukua jukumu la tume hiyo ya walinda amani mwezi ujao, kulinda raia na kurejesha uthabiti wa serikali kuu. |