EMMANUEL MSUYA ANYAKUA MILIONI HAMSINI ZA EPIQ BONGO STAR SEARCH

mshiriki wa kiume pekee aliyeingia katika fainali za shindano la uimbaji wa muziki la Epiq Bongo Star Search Emmanuel Msuya Ameibuka Mshindi Wa Taji Hilo Baada Ya Kuwaburuza Wenzie Kwa Kura Zilizokua Zikipigwa Na Mashabiki Waliokua Wakifatilia Shindano Hilo Kwa Ukaribu Tangu Lianze.
Awali Washiriki Wote Watano Walianza Kwa Kuimba Nyimbo Zao Walizorekodiwa Wakiwa Ndani Ya Shindano Hilo Kwa Waandaji Nguli Wa Muziki Akiwemo Shirko, Lamar Wa Fishcrab Na Sheddy Clever Wa Burn Records.
Katika Raundi Hiyo Ya Kwanza,Mshindi Wetu Wa Epiq Bongo Star Search Kijana Emmanuel Msuya Aliimba Wimbo Wake Uliobeba Jina La "Leo Ni Leo" Wakati Mwenzie Aliyetinga Nae Hadi Mbili Bora Na Pia Ndiye Mshindi Namba Mbili Aliimba Wimbo Wake Aliouita "Moyo Unadunda "
Huku Washiriki Wengine Wakiwa Top 5 Ambao Pia Nao Walishiriki Raundi Hiyo Ni Pamoja Na Amina Chibaba Aliyeimba Wimbo Wake Unaoitwa "Nalia Na Moyo" Maina Thadei Aliyetamba Raundi Hiyo Kwa Wimbo Wake Aliouita "Panya Buku" Huku Malisa John Aliyetamba Pia Katika Raundi Hiyo Na Wimbo Wake Alioupa Jina La "Mapenzi Ya DalaDala"
Raundi Iliyofata Wasanii Wote Walipewa Nafasi Ya Kuimba Nyimbo Za Wasanii Wengine Ambapo Amina Chibaba Akaimba Wimbo Wa "Mwansiti",Elizabeth Mwakijambile Akaimba Wimbo Wa Awilo Longomba Unaoitwa "Kalorina"Huku Mshindi Wa Mwaka Huu Emmanuel Msuya Akaimba Wimbo Wa Diamond Musica Band Unaoitwa "Mapenzi"Pia Maina Thadei Akaimba Wimbo Wa Miriam Makeba Unaoitwa "PataPata"Na Akamalizia Melisa John Na Wimbo Wa Mariah Cary Unaitwa "Heroe"
Hatua Ya Tatu Washiriki Wawili Walitoka Kutokana Na Ufinyu Wa Kura Zao Ambapo Washiriki Kama Amina Chibaba Pamoja Na Maina Thadei Waliyaaga Mashindano Huku Elizabeth Mwakijambile,Emmanuel Msuya Na Melisa John Walitinga Tatu Bora Na Kuendelea Na Mpambano Ambao Haukuonekana Kua Mrahisi
Raundi Ya Mwisho Ambayo Ni Ya Nne Chini Ya Jopo La Majaji Watano Akiwemo Chief Jaji Madam Ritha,Master J,Fid Q,Banana Zoro Pamoja Na Barnaba Kutokana Na Uchache Wa Kura Za Mshiriki Melisa John Wa Ukonga Jijini Dar Es Salaam Ilimlazimu Kuaga Mashindano Hayo Huku Akiwaachia Ulingo Elizabeth Na Emmanuel Ambapo Nyota Ya Mshindi Huyo Wa Ebss 2013 Ilianza Kuonekana Baada Ya Kupanda Jukwaani Na Kupokelewa Na Watu Vizuri Akiwa Anaimba Wimbo Aliouchagua Katika Raundi Hiyo Ya Mwisho Unaojulikana Kama "Maneno Maneno" Wa  Msanii Maarufu Anayesumbua Sana Katika Industry Ya Muziki Wetu Anayefahamika Kama BenPol Na Kupelekea Kumfunika Mwenzie Mwanadada Elizabeth Sio Tu Kwenye Stage Bali Hata Kwa Kura Zilizokuwa Zikipigwa Usiku Huo
RED CARPET ILIKUA HIVI
DSC_0002
DSC_0006
DSC_0004
DSC_0006
DSC_0015
DSC_0018
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family