William J Mtitu |
Stori: Jelard Lucas
STAA wa sinema za Kibongo, William Mtitu amewatemea cheche wasanii
wenzake kwa kuwaambia kupata tuzo ndiyo silaha ya mafanikio kwa mastaa
wa sinema Bongo hivyo wasanii wanaolewa umaarufu pasipo kuwa nazo, ni
kazi bure.
Akizungumza na paparazi wetu, Mtitu alisema huwa anafurahi kuingia
katika tuzo mbalimbali na mwaka huu ameingia katika mchakato wa Magic
Swahili Movies Award 2013 akiamini atashinda na kujijengea heshima.
“Tuzo ni za Magic Swahili Movies 2013 ni nguzo kwa wasanii kwani
zinasaidia kuonesha umetoka wapi na unaelekea wapi, nimeingia kwenye
kipengele cha Muongozaji Bora na Filamu Bora ya Mwaka,” alisema Mtitu.