WAFANYAKAZI WA REDCROSS WATEKWA


Wafanyakazi wa Red Cross wakiwa kazini Syria.

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC) limesema watu wenye silaha wamewateka wafanyakazi sita wa shirika hilo na mfanyakazi mmoja wa kujitolea wa shirika la Mwezi Mwekundu huko kaskazini-magharibi mwa Syria.
Shirika hilo limesema halijapata mawasiliano yoyote na wateka nyara hao, kwa mujibu wa msemaji wa ICRC.
Awali, vyombo vya habari vya serikali ya Syria vilieleza kuwa watu hao wenye silaha walishambulia wafanyakazi wa Red Cross waliokuwa wakisafiri kwa gari kati ya Sarmin na Saraqeb kwenye jimbo la Idlib.
Shirika la ICRC limesema limekuwa likipata ugumu wa kuyafikia maeneo mengi ya Syria kufikisha misaada kwa watu waliojeruhiwa au kuyakimbia makazi yao.

 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family