Romelu Lukaku ameisaidia timu ya taifa ya Ubelgiji kufuzu kwenye fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil.
Magoli 2 yaliyotiwa kimiani na mshambuliaji huyo wa Chelsea yaliipatia ushindi Ubelgiji ikichezea ugenini dhidi ya Croatia.Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 25 sasa anaichezea Everton kwa mkopo kutoka Chelsea.
Alishinda magoli hayo katika kipindi cha kwanza,huku goli la kufutia machozi la Croatia likifungwa na Niko Kranjcar dakika chache kabla ya mechi kumalizika.
Timu ya taifa ya Ubelgiji inaongoza kundi A ikiwa na alama 25.inaizidi kwa alama 8 Croatia ambayo inashikilia nafasi ya pili.
Katika kundi B Italia imetoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Denmark ,lakini Italia imekwishafuzu.
Timu nyingine zilizofuzu ni Ujerumani,Uholanzi na Uswiss.Ugerumani katika kundi la C iliilaza Ireland magoli 3-0.Uholanzi iliinyeshea Hungary mabao 8-1 yakiwemo 3 yaliyofungwa na mahsmabuliaji wa Manchester United Robin Van Persie na Uswiss ikichezea ugenini iliifunga Albania mabao 2-1.