Katibu
Mkuu wa Wizara ya Sayansi Tekinolojia na Mawasiliano Profesa Patrick
Makungu akifungua semina ya siku tatu inayokutanisha Wataalamu
mbalimbali wa TEHAMA kutoka nchi za (SADC) zinazounganishwa na taasisi
ya Southern Africa Telecommunications Association.
(SATA)
ili kujadili namna ya kuzuia Wizi na uhalifu kupitia kwenye mtandao
(Fraud Management, Revenue Assurance and Network/Cyber Security)
inayofanyika kwenye hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam
ikishirikisha makampuni ya simu katika nchi za kusini mwa Afrika, Katika
semina hiyo kumeripotiwa wizi wa fedha unaofikia asilimia 8% mpaka 13%
ikiwa ni pamoja na uhalifu mwingine, Semina hiyo imeandaliwa kwa pamoja
na Kampuni ya Simu ya TTCL ikishirikiana na Taasisi ya Southern Africa Telecommunications Association. (SATA)Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya TTCL Dr. Kamugisha Kazaura akizungumza
katika semina hiyo wakati akiwakaribisha washiriki wa semina hiyo
inayofanyika kwenye honteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam.
Jacob Munodawafa Katibu Mkuu wa taasisi ya Southern Africa Telecommunications Association.(SATA) akizungumza katika semina hiyo wakati akizungumzia malengo ya SATA kufanya semina hiyo kwa wadau wake.