skip to main |
skip to sidebar
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
WILAYA YA MBOZI – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 16.10.2013 MAJIRA YA SAA 22:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHENJE
KATA YA MYOVIZI, TARAFA IYULA, WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. MTU
MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA
MIAKA 20-25, ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA MWILI
WAKE KUTUPWA KWENYE SHAMBA MALI YA FRIDAY S/O BUKUKU. CHANZO
KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA JERAHA UBAVU WA KULIA,
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE.
WILAYA YA MBOZI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 16.10.2013
MAJIRA YA SAA 02:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISALALO, KATA YA MSIA,
TARAFA YA IGAMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. TUSAMALE S/O MWILEGA,
MIAKA 70, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA ISALALO ALIFARIKI DUNIA AKIWA
AMELALA NDANI YA NYUMBA YAKE BAADA YA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KUCHOMA
MOTO NYUMBA YAKE. MAREHEMU ALIKUWA ANAISHI PEKE YAKE KATIKA NYUMBA HIYO
ILIYOJENGWA KWA MATOFALI MABICHI NA KUEZEKWA KWA KUTUMIA NYASI. CHANZO
KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA
NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA
MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA