Marehemu Julius Nyaisanga Enzi Za Uhai Wake |
Pichani
kati ni Marehemu Julius Nyaisanga akiwa na wadau enzi za uhai
wake,pichani kulia ni Othman Michuzi na shoto ni Aboubakary Lyongo
Mtangazaji
mkongwe hapa nchini,aliyekuwa Meneja wa Aboud Media, Julius
Nyaisangah,ambaye pia alikuwa mtangazaji wa Radio One na ITV, amefariki
dunia leo majira ya saa moja asubuhi katika hospitali ya Mazimbu Mkoani
Morogoro.
Taarifa za awali zinasema kuwa marehemu Nyaisanga alikuwa anasumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu pamoja na kisukari.
Wakati
wa uhai wake, marehemu Nyaisanga aliwahi kufanya kazi sehemu mbali
mbali ikiwemo katika makampuni ya IPP ambako alikuwa mkurugenzi wa Radio
One pamoja na Radio Tanzania wakati huo ikiitwa RTD ambako alikuwa
mtangazaji wa vipindi mbali mbali. Marehemu ameacha mjane na watoto
watatu.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.