UFOO SARRO |
.
Awali
taarifa zilizosikika katika vyombo vya habari vya ipp ambapo Ufoo
anafanyia kazi zilisema kuwa Mwandishi wa habari wa Kituo Cha Habari
cha
ITV na Radio One UFO SARO amepigwa risasi mbili na anayesemekana kuwa ni
Mchumba Wake aliyekuwa akifanya Kazi Sudan Kupitia UN.
Sababu ya
Kupigwa Risasi yeye UFO SARO na Mama yake Mzazi Ufo Saro ambaye
amepoteza maisha papo hapo ni ugomvi ambao haujajulikana na huku
Aliyewapiga risasi UFO SARO pamoja na Mama yake Mzazi Ufo kajipiga
risasi chini ya kidevu na kupoteza maisha papo hapo..
Habari
zilizotufikia hivi sasa zinasema Ufoo kwa sasa amehamishiwa katika
chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) Kwa uangalizi zaidi.
tuendelee
kumuombea ili apate unafuu na arejee katika kazi zake za kila siku za
kuhabarisha umma.tutaendelea kuwahabarisha zaidi kwa kadri tutakavyokuwa
tunapata taarifa kuhusu hali yake.