Kiungo
wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima ambaye pia ni
mchezaji wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom wa timu ya Young Africans
amepatwa na jangwa la kuunguliwa kwa baadhi ya mali zake kufuatia
kutokea shoti ya umeme leo asubuhi.
Niyonzima ambaye anaishi eneo la Magomeni Makuti amekutwa na na
tatizo hilo leo asubuhi majira ya saa 12 akiwa anajiandaa kuelekea
mazoezini ndipo alipoona moshi ukifuka kutokea eneo la sebuleni kwake na
aliposogea alibani ni moto ulikuwa ukiwaka.
"Nilisikia hewa nzito
ndani, nikaamka kuelekea sebuleni, nilipofika nilikuta moto umetanda
chumba kizima ndipo majirani walijitokeza na kuanza kutusaidia kuzima
moto huo kwa kuvunja madirisha ya vioo na kumwaga maji ili moto huo
uzime" alisema Niyonzima
Nashukuru tulifanikiwa kuuzima moto
baada ya muda kwa kushirikiana na majirani lakini vitu vyote vilivyokuwa
ndani hatukufanikiwa kuivitoa vikiwa salama, baadhi ya vitu
vilivyoungua ni pamoja na Luninga iliyokua imefungwa ukutani, redio
(music system), makochi na fenicha za ndani.
Aidha Niyonzima
amesema moto huo utakua umetokana na shoti ya umeme juu ya dali kwani
ndio sehemu inayooenekana kuwa chanzo cha moto.
Afisa Habari wa
klabu ya Yanga SC Baraka Kizuguto alifika nyumbani kwa Niyonzima majira
ya saa 2 kasorobo asubuhi kuongea na mchezaji ambaye alisema anashukuru
familia yake wote wako salama na hakuna aliyedhurika zaidi ya vitu
vilivyoteketea na moto.
Uongozi wa klabu ya Yanga SC unampa pole
Niyonzima kwa matatizo yaliyomfika, Mungu amjalie nguvu na uvumilivu na
kusema upo nae pamoja katika wakati huu mgumu.