Msafara
wa magari yakipita katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana
kuitangaza kampeni ya Nani Mtani Jembe inayowashindanisha mashabiki wa
Simba na Yanga kuzipa shavu timu zao kupitia kampeni hiyo inayoendeshwa
na Kilimanjaro Premium Lager. Msafara huo utatembelea maeneo mbalimbali
ya jiji la Dar es salaam kwa siku tatu.
Mashabiki
wa Simba na Yanga wakiwa wanacheza kwa furaha jana wakati wa maandamano
maalum yaliyofanywa kuitangaza Nani Mtani Jembe inayoendeshwa na
Kilimanjaro Premium Lager kwa mashabiki wa jiji la Dar es salaam.
Msafara huo utatembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kwa
siku tatu kuitambulisha kampeni hiyo na kutoa elimu namna ya kushiriki.
Mashabiki
wa Simba na Yanga katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam leo
wamepokea kwa kishindo promosheni ya Nani Mtani Jembe inayoendeshwa na
bia ya Kilimanjaro Premium Lager nchi nzima kwa siku 75 ili kuleta
mwamko katika utani wa jadi kati ya mashabiki hao.
Kampeni
hiyo ilipokelewa kwa kishindo baada ya wafanyakazi wanaoitangaza
kampeni hiyo wakiwa na msafara wa magari kutembelea maeneo mbalimbali ya
jiji hususani yale ambayo ni maarufu kwa kuwa na mashabiki au makundi
maarufu ya ushabiki kama vile Wakali wa Terminal, Vuvuzela Tandale, nk
pamoja na vijiwe na matawi ya Simba na Yanga na kutoa burudani na
maelezo ya kushiriki pamoja na kuitambulisha rasmi mtaani kampeni hiyo
ya aina yake.
Baadhi
ya wafanyabiashara katika soko la Tandika wilaya ya Temeke walisema
kuwa kampeni ya Nani Mtani Jembe imeleta mwamko mkubwa sana katika utani
wa jadi uliopo kati ya mashabiki wa Simba na Yanga na pia wanaamini
itasaidia kuwaleta karibu zaidi mashabiki pamoja na kuibua mashabiki
wapya.
“Jonathan
Assey alisema “Nimeanza kushabikia Yanga tangu nikiwa na miaka 14
lakini sijawahi kuona tukio lolote kubwa la kusisimua namna hii ambalo
ni mahususi kwa ajili ya mashabiki, hivyo nawashukuru Kilimanjaro
Premium Lager kwa kutukumbuka sisi mashabiki na kutuletea hii kampeni”.
Meneja
wa Bia ya hiyo, George Kavishe alisema jana kuwa katika shindano hilo
Kilimanjaro inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha
shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu
inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Kavishe
alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa
kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata
fedha nyingi zaidi ya timu nyingine.
Akielezea
namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa
shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la Nani Mtani
Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni
kununua bia ya Kilimanjaro ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya
kushiriki.
Alisema
baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye
kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na
kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia
kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.
Alisema
baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 1,000
kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa
Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 1,000 kutoka kwenye fungu
la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza shilingi
1,000 kutoka kwa Simba.
Kwa
mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba
au Yanga yatangazwa kila siku kuanzia leo Jumatatu hadi siku ya mwisho
wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu.
Kavishe
alisema kuwa mashabiki watakaoshiriki kwenye shindano hilo kila siku
pia watanufaika kwa kuchaguliwa watu 400 watakaokuwa wametuma mara
nyingi zaidi ambao pia watazawadiwa shilingi 5000 kila mmoja na kufanya
kiasi cha fedha zinazokwenda kwa mashabiki kuwa shilingi milioni mbili
kila wiki.
Mashabiki wanaweza kufatilia matokeo kila dakika kupitia tovuti maalum ya Nani Mtani Jembe ambayo ni https://cms.rasello.com/kili.