BALOZI SEPETU ( BABA MZAZI WA WEMA) AZIKWA

 Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,ukitemshwa katika kaburi wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo,  alipowasili katika eneo la Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa na viongozi wengine akiwemo Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Mohamed Gharib Bilali,katika Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja leo
  Jeneza la Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,likiwa limebebwa na Askari Polisi na kulifikisha katika kaburi lake yalipofanyika mazishi kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja leo.
 Padri wa Kanisa Katoliki la  Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, akiuombea mwili wa marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja leo.
Msanii Wa Kizazi Kipya ( Aliyevalia kanzu Nyeusi ) Diamond Platnumz Hakuwa Nyuma Kuhudhuria Msiba Wa Aliyekuwa Baba Wa Mpenzi Wake Wa Zamani Wema Isaac Abraham  Sepetu




 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family