Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Jumanne jioni ametangaza kuwa operesheni
za kijeshi dhidi ya magaidi zimemalizika katika maduka ya kifahari ya
Westgate Mall jijini Nairobi.
Rais Kenyatta alisema Kenya imewaaibisha washambuliaji hao, kuwauwa magaidi watano na kuwakamata wengine 11 ambao wamezuiliwa. Alisema takriban watu 61 wamethibitishwa kufa tangu magaidi hao walipovamia maduka hayo Jumamosi.
Msako huo uliingia siku ya nne leo Jumanne huku jeshi la ulinzi la Kenya KDF likisema linaudhibiti wa maduka hayo. Watu 240 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.
Rais huyo wa Kenya pia ametangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuataia shambulizi hilo.