MWANA FA BAADA YA KUPEWA KASHFA ZA AHADI HEWA,MAMA MANGWEHA AKANUSHA HABARI HIZO NA KUSEMA ALITIMIZIWA AHADI

fa

Kutokana na tuhuma ambazo watu wengi walimpa Mwana F.A kwamba alitoa ahadi hewa kwenda kwa Mama Mangwea. Kwenye show ya The Finest, Mwana F.A aliahidi kutoa asilimia 15 za faida ya onyesho hilo. Akiongea na Mwananchi alisema,“Nakiri kukosea jambo moja, nilipoahidi niliongea na wanahabari lakini wakati wa kutoa nilitoa bila kutangaza.Hii kutoa jamani ni moyo, haina haja kumtangaza mtu kwa kuwa umemsaidia au umempa pole”.
Upande wa pili Mama Mangwea alipoulizwa alisema,“Kabla hata ya arobaini, aliweka benki kisha akaja na mwenyewe, hakuna na waandishi kama wanavyofanya wenzake. Alikuja mwenyewe tukaongea na mara kwa mara tunawasiliana, wanataka kumtia doa kijana wa watu ni muungwana sana”.
Source : Mwananchi
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family