Ikiwa ni
miaka miwili tu tangu kuwekeza kwenye mfumo wa simu wa kampuni kubwa ya
tarakilishi, Microsoft (Windows Phone), kampuni iliyovuma sana kwenye
soko la simu za mkononi, Nokia, imeangukia moja kwa moja mikononi mwa
Microsft kwa kukubali kuuza simu zake kwa jumla ya euro bilioni 5.44
(sawa $7.2 bilioni).
Nokia, kampuni tanzu ya Ufini (Finland) imekubali Microsoft, kampuni tanzu ya Marekani, kuipa umiliki wa simu za kisasa zinazotumia mfumo wa Lumia ambao unatumika kwenye mfumo wa simu za Windows za Microsoft.
Microsoft italipa $5 bilioni kununua vifaa na huduma za Nokia na itaongeza $2.2 kusajili ‘patent’ za Nokia. Biashara nzima inatarajiwa kufungwa rasmi mwanzoni mwa robo ya kwanza ya mwaka 2014 ikiwa wadau na wasimamizi wataafiki.
Kampuni hizo kubwa zimekuwa zikifanya kazi kwa ushirika wa karibu tangu mwezi Februari mwaka 2011 kwa

malengo ya
kutengeneza simu za kisasa ambazo zingepambana na simu za kisasa za
kampuni za Apple (Marekani) na Samsung (Korea Kusini).
Nokia ni kampuni yenye umaarufu zaidi katika nchi za mabara ya Ulaya, Afrika na Asia lakini bado imeshindwa kujipenyeza hivyo kwenye soko la Marekani ingawaje imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupiku soko linalosua sua la BlackBerry na kuchukua nafasi ya tatu kwenye makampuni makubwa ya simu za kisasa.
Jisomee taarifa ya Microsoft kwa umma kuhusu hilo (kwa kubofya hapa) Text of Microsoft's news release about the deal na barua ya Mkurugenzi wa Microsoft, Ballmer, Elop (kwa kubofya hapa) Text of blog post from execs
Wadadisi wa mambo wanasema hatua hii ya Microsoft kuinunua Nokia inaashiria kuwa imenuia kuwa kampuni ya kutengeneza vifaa hivyo zaidi (more of a devices company) ya kutengeneza mifumo ya kuenesha vifaa vyenyewe (less of a software company).
Hii ni mara ya pili kampuni ya Microsoft inatoa kiasi kikubwa kabisa cha fedha na kununua sehemu ya kampuni nyingine kubwa, baada ya kufanya hivyo mwezi Mei 2011, ilipoinunua kampuni ya simu za kwenye iternet, Skype kwa kiasi cha $9.3 bilioni.
Yaelekea ndoto zake ni kubwa kwani iliota kuhakikisha kuwa inaweka kompyuta katika kila meza ya ofisi na sasa inanuia kuweka simu katika kila mfuko wa nguo. Ikiwa itafanikiwa ama itafeli, walengwa tunasubiri kujionea.