ZAIDI ya sh. bilioni 881, zitatumika katika mradi wa kusambaza umeme vijijini na
kuwanufaisha zaidi ya wateja
250,000.Mwenyekiti wa
Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Balozi Ami Mpungwe, aliyasema
hayo Dar es
Salaam jana baada ya kusaini mikataba 15 ya utekelezaji wa miradi ya
kusambaza
umeme vijijini awamu ya pili.
Alisema lengo
la mradi huo ni kusambaza umeme katika mikoa 24 ya Tanzania Bara
hususani
vijijini na kwenye Makao Makuu ya Wilaya 13 zisizo na umeme."Utekelezaji
wa
miradi katika mikoa 14 iliyopata makandarasi, unaenda sambamba na ujenzi wa
vituo sita
vya usambazaji umeme ambavyo vitajengwa Tunduru, Mbinga, Ngara,
Kigoma, Kasulu na
Kibondo," alisema Balozi Mpungwe.
Alitaja mikoa
iliyopata makandarasi kuwa ni Ruvuma, Arusha, Dodoma, Mara, Iringa,
Kilimanjaro, Singida Mtwara, Mwanza, Tabora, Njombe, Katavi, Shinyanga na
Simiyu
ambapo
mikoa 10 haijapata makandarasi."Katika
kutekeleza miradi hii, huduma za kijamii kama
shule,
zahanati na visima vya
maji vitapewa kipaumbele kwa kuunganishiwa umeme," aliongeza.
Wakati
huo huo, Balozi Mpungwe aliwataka wakandarasi wote kuhakikisha
wanasimamia na
kutekeleza wajibu wao kulinganana mikataba na wale ambao
watakwenda tofauti hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Alisema
asilimia 98 ya vijiji vilivyopo nchini, vina matatizo ya kupata umeme usio na
uhakika
hivyo kuanzishwa kwa REA, kumesaidia ongezeko la upatikanaji umeme
katika maeneo hayo
kwa asilimia saba ukilinganisha na awali ambapo asilimia 2.5
ya wananchi waishio vijijini ndio
waliokuwa wanapata umeme.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa REA, Bw. George
Nchwali, alisema Utekelezaji wa Mpango
Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini ni
sehemu ya juhudi za Serikali kufanikisha Mipango
ya Maendeleo ya Taifa kama
ilivyoainishwa katika Dira ya Maenedeleo ya Taifa kufikia
asilimia
30 wa
wananchi waishio vijijini, wanapata umeme ifikapo mwaka 2015