Leo kupitia ukurasa wake wa twitter, mbunge wa
Jimbo la Bumbuli kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mheshimiwa January
Makamba ameandika ujumbe ambao kama kweli unaweza kufanyiwa kazi basi
unaweza kuwainunua “milele” kiuchumi wasanii wetu wa filamu nchini na
kuwawezesha kuondokana na hali ya vipato duni dhidi ya kazi zao kubwa
wanazozifanya za uelimishaji wa jamii kupitia sanaa ya uigizaji na
filamu.
Katika ujumbe huo Mheshimiwa makamba ametoa takwimu hizi kama ifuatavyo.
“There're 130 mil Swahili speakers. If only 1% buy a Bongo movie
at Sh 5,000/=, that's Sh 6.5 billion. If an artist gets 20%, that's 1.3
bil”
Akimaanisha kuwa;-
Kuna karibu watu milioni mia moja na Thelathini (130 mil)
wanaozungumza Kiswahili. Kama angalau asilimia moja ya watu hao milioni
mia moja na thelathini – yaani watu milioni moja na laki tatu
(1,300,000) wakinunua filamu hizo kwa shilingi elfu tano tuu kwa filamu
moja, itapatikana shilingi bilioni sita na nusu (6.5 bil) toka kwenye
mauzo hayo- na kama msanii atapata angalau asilimia ishirini (20%) ya
mauzo hayo basi atajipatia shilingi bilioni moja pointi tatu (1.3 bil) - pesa ambazo kiukweli zitamkomboa kabisaaa kwenye umaskini.
Je, maoni haya anweza kuwa kweli? Kama ndiyo ni kitu gani kifanyike basi? Tupe maoni yako.