ARUSHA.
MAZISHI ya kifahari yanaandaliwa na familia ya marehemu Erasto Msuya, huku ikielezwa kuwa jeneza litakalotumika kubeba mwili wake linafunguka kwa kutumia ‘rimoti’.
MAZISHI ya kifahari yanaandaliwa na familia ya marehemu Erasto Msuya, huku ikielezwa kuwa jeneza litakalotumika kubeba mwili wake linafunguka kwa kutumia ‘rimoti’.
Msuya aliyeuawa wiki iliyopita, anazikwa leo huku
familia ikitangaza kutokulipiza kisasi kwa waliohusika, badala yake
wamemwachia Mungu.
Kinachovutia katika msiba huo ni jeneza lililobeba
mwili wa mfanyabiashara huyo lililoagiz
wa Nairobi, la aina yake huku likifunguliwa kwa kutumia ‘rimoti’.
wa Nairobi, la aina yake huku likifunguliwa kwa kutumia ‘rimoti’.
Jeneza hilo lililoagizwa kutoka Kampuni ya
Montezuma & Monalisa Funeral Home, linafunguliwa kwa kubonyeza kifaa
maalumu hata mhusika anapokuwa mbali.
Hali hiyo ilionekana kuwaacha na mshangao maelfu
ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wakati wa ibada iliyofanyika
nyumbani kwake, Kwa Iddi, wilayani Arumeru.
Mfanyabiashara huyo aliyeuawa kwa kumiminiwa
risasi zaidi ya 20 na watu wasiojulikana, anazikwa leo nyumbani kwao
eneo la Kairo Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.
Kaka wa marehemu, Israel Msuya, alisema jana kuwa
mazishi hayo yatafanyika makaburi ya familia ya mzee Elisaria Msuya
‘Kikaango’, baba wa marehemu Erasto.
Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya mazishi hayo
inayoongozwa na kaka mkubwa wa familia ya Msuya, Gady, zaidi ya Sh100
milioni zimepangwa kugharimia shughuli za maombolezo na mazishi.
Jeneza na gari maalumu la kubebea mwili wa
marehemu yameagizwa kutoka Kampuni ya Montezuma & Monalisa Funeral
Home ya Nairobi, Kenya kwa gharama ya Sh8 milioni.
Chakula, vinywaji, mapambo na magari ya kukodishwa
kutoka Arusha kwenda Mirerani na kurudi yanatarajiwa kugharimu zaidi ya
Sh80 milioni.
Katika hatua nyingine, polisi mkoani Arusha
imeendelea kuwahoji wafanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite wa
Mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro, wakidaiwa kuhusika na kifo
hicho.
Habari zilizopatikana jana zinadai mfanyabiashara
mmoja kijana ambaye aliibuka ghafla kuwa tajiri mkubwa kutokana na
biashara ya madini ya Tanzanite, anashikiliwa Arusha kwa mahojiano. MWANANCHI