HUYU NDO TRAFIC POLICE FAKE ALIYEKAMATWA LEO TABATA KINYEREZI

Umri wake haujatajwa lakini anaonekana ni mtu mzima, amekamatwa Tabata Dar es salaam August 14 2013 mchana baada ya kushtukiwa.
Kuna polisi wa kweli waliambiwa na Wananchi kwamba kuna askari wa usalama barabarani anatoza faini kwa madereva mbalimbali anaowakamata, anacho kitabu yani akikumata anakuandikia faini kabisa.
Hapo ndipo alikua anapiga hela nyingi manake faini unaambiwa inaanzia elfu 20 mpaka elfu 25 na kuendelea kulingana na idadi ya makosa.
Wananchi walipotoa taarifa baada ya vitendo vya huyu mzee kuzidi, Polisi wakatumia siku tatu kumchunguza…. siku nyingine walikua wanamkuta Tabata na pia alikua ana chimbo lake jingine Mkuranga.
Alipokamatwa amekutwa na kitabu cha kutoza faini, analo koti linalovaliwa na Mapolisi barabarani usiku lile linalowakawaka na pia kakutwa na hizo jezo za Askari haijulikani hata kazipata wapi pamoja na vifaa vingine.
Polisi inaendelea na uchunguzi.


Traffic Fake Akiwa Tayari Yupo Chini Ya Ulinzi

Afande huyo akiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa mchana wa leo akila vichwa maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam.Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake. - See more at: http://williammalecela.blogspot.com/2013/08/trafiki-fake-anaswa-sitakishari-ukonga.html#sthash.wc7NfgDm.dpuf
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family