Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. |
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetangaza kutoa
donge nono la shilingi milioni 100/= kwa mtu yeyote atakayewezesha
kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo
vya kuwamwagia na kuwadhuru watu kwa tindikali.
Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman Kova amesema: “Nimeamua kuomba
fedha hizi serikalini ili nimpe mtu atakayewezesha kupatikana kwa
taarifa hizo, hatimaye kukomesha vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na
madhara makubwa.”